Lebo maarafu nchini Wasafi Classic Baby ‘WCB’ inayomilikiwa na mwanamuziki nyota nchini, Diamond Platnumz inatarajia kufungua ofisi mpya Kijitonyama jijini Dar es salaam ambayo itakuwa inajihusisha na masuala ya kiuongozi tu.

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam amesema wanafungua ofisi mpya ili kuipa nafasi ofisi ya zamani ya kufanya shughuli zake bila kuingiliana na shughuli zingine.

Pia amesema ofisi hiyo itakuwa kwa ajili ya viongozi tu huku ofisi ya mara ya kwanza itaendelea na kazi nyingine kama kawaida.

WCB ni moja kati ya label za muziki ambazo zinafanya vizuri kutokana na wasanii wake wengi kufanya vizuri katika anga ya muziki nchini.

Lebo hiyo inajumla ya wasanii wanne ambao ni Diamond Platnumz anayeongoza kundi hilo pamoja na Harmonize, Raymond na Rich Mavoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *