Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Mstaafu, Joseph Nkaissery amefariki dunia.

Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.

“Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,”.

Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekwua seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *