Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres amemtangaza Amina Mohammed kuwa naibu wake.
Guterres ametangaza uteuzi wa wanawake wengine wawili kwa nyadhifa za juu katika Umoja wa Mataifa.
Guterres ametoa tangazo hilo kupitia kwa msemaji wake Stephane Dujarric.Bi Amina Mohammed ni waziri wa mazingira wa Nigeria.
Pia alifanya kazi kama msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeondoka Ban Ki-Moon, kwenye ajenda ya maandeleo ya mwaka 2030.
Lakini serikali ya Nigeria bado haijasema kuwa imejulishwa kuhusu uteuzi huo.
Mkuu huyo mpya wa Umoja wa Mataifa ataingia ofisini Januari mosi mwaka 2017 kwa kipindi cha miaka mitano.