Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018.

Waziri huyo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti leo.

Katika bajeti hiyo Serikali inatarajia kuajiri watumishi 4,339 katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Wakati huo huo, Nchemba alisema Serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi Rufiji ili kukabiliana na uhalifu katika maeneo hayo.

“Kutokana na ongezeko la matukio makubwa ya uharifu katika Wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji, katika mwaka 2017/18, Serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi Rufiji.

Akizungumzia uhakiki wa silaha ambazo baadhi zimekuwa zikitumika katika uhalifu, waziri huyo alisema hadi kufikia Machi mwaka huu, asilimia 63.2 ya silaha hizo zilikuwa zimehakikiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo, aliitaka Serikali iimarishe ulinzi katika wilaya za mkuranga, Kibiti na Rufiji ili wananchi wa maeneo hauo waweze kuishi kwa amani.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *