Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa watuhumiwa wa wa makinikia walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzuia serikali iache kufatilia sakata hilo.

Nchemba amesema kuwa “Wale wenye nia mbaya wametafuta vichaka vingi sana lakini kila kichaka wakijaribu na chenyewe kinayeyuka, walisema tutashtakiwa hivi siku hizi mwizi naye anashtaki aliyemwibia?

“Mwanzoni walikuwa wanasema mchanga tu hauna kitu lakini hili wala halihitaji shule kujua kama ni mchanga tu hauna kitu hawa watu wangekuwa wanakuja kuchukua mchanga tu kila siku.

Kwa hiyo hawa watu walikuwa wanatuona kama mazuzu tu lakini Rais wetu amechukua hatua tena si kwa maneno kwa vitendo tumuunge mkono”.

“Walipoona kichaka hicho kimekwama wakaanza kutaja viongozi kuwa wanahusika wakidhania hiyo itakuwa kitu cha kuzuia ili jitihada hizo zisiendelee wakaanza kutaja na viongozi wastaafu hiyo yote si kama walikuwa wanataja kuwa viongozi hao wanahusika bali walikuwa wanataka itumike kama kichaka kwamba tukitaja viongozi hao wataacha.

“Mimi niwaambie viongozi wetu hawa hawajawahi kuwa Ma- Agent wa wale wanaotuibia bali wale wanaotetea wezi ambao tumewaona ndiyo Ma- Agent wa wezi hao, na Rais akauona huo mtego akautegua sasa hivi kama ni gari lao lile basi matairi yote Rais Magufuli ameshatoa upepo, yameshalala chini” alisema Mwigulu Nchemba.

Waziri Mwigulu aliyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa ya Ndago katika mwendelezo wa ziara jimbo kwake Iramba Magharibi mkoani Singida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *