Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemtaka Ofisa Utawala Mkuu wa Uhamiaji kueleza sababu zilizofanya askari polisi wapya 297 kushindwa kulipwa mishahara yao katika kipindi cha miezi minne.

Waziri Nchemba amesema wakati akiwa bungeni aliulizwa swali la kwanini askari hao walishindwa kulipwa mishahara yao katika kipindi cha miezi minne.

Amesema kutokana na askari kutokuwa na tabia ya kulalamika mara kwa mara, wamekuwa wakiwacheleweshea mishahara yao na hata kutoongezewa pindi wanapopandishwa vyeo na kufanya kuwa kigezo cha wao kuwa na sababu mbalimbali za kusingizia.

Nchemba amesema amegundua maofisa utawala kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani wamekuwa tatizo kubwa baada ya kutembelea idara mbalimbali zilizopo chini ya wizara hiyo.

Naye Ofisa Utawala Mkuu wa Uhamiaji, Mulegi Majogoro, amesema mishahara ya askari wapya ilishindwa kutolewa kwa sababu ya kuwapo kwa makosa mbalimbali katika vyeti vyao.

Amesema baadhi ya vyeti vya askari hao vilikuwa na tofauti ya majina pamoja na miaka jambo lililosababisha kushindwa kulipwa mishahara yao kwa miezi minne kutokana na kuvichunguza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *