Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amevitaka vyombo habari kuwa chachu ya mabadiliko katika kipindi hiki nchi inaelekea katika uchumi wa kati.

Nape ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya vyombo vya habari vya Clouds Media, Azam na Mlimani ziara ambayo inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na sekta ya habari nchini.

Waziri Nape amesema kumekuwa na mitazamo tofauti katika vichwa wa wananchi au jamii kwa ujumla katika suala zima la kuelekea uchumi wa kati hivyo ni jukumu la vyombo vya habari nchini kuweza kuwaelimisha wananchi kuhusu suala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *