Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio vya Radio 5 na Magic FM kwa muda usiojulikana kurusha matangazo yao.

Waziri Nape ametangaza uamuzi huo hivi punde katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuzitaja redio hizo kuwa ni Radio 5 FM ya Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape amesema kwamba adhabu hiyo ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo Agosti 29 mpaka kamati ya uchunguzi itakapomaliza kazi yake..

Pia amesema sababu ya kuvifungia vituo hivyo kutokana na nyakati tofauti na katika vipindi vyao tofauti walitangaza habari zilizokuwa na uchochezi ambazo zinaweza kuvuruga amani ya nchi.

Nape amesema amewasiliana na kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuwahoji wahusika na kisha kushauri adhabu ambazo zitakazofaa dhidi yao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *