Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amepinga zuio la TCRA kuzisimamisha Online TV kwa kuwa kanuni zinazotoa muongozo bado zipo kwenye mchakato hazijakamilika.

Nape ametengua katazo hilo baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzipiga marufuku Online TV.

Waziri huyo alifafanua kuwa ni lazima uendeshaji wa maudhui ya mitandaoni kwa wana habari ifuate kanuni na sheria na kwamba kanuni zinazokuja hazitakuwa na nia ya kuzuia bali kusimamia (regulate).

Amesema nia ya kuweka kanuni hizo ni kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji wa watumiaji wa maudhui ya mtandaoni na wanaoweka maudhui hayo na kwamba utaratibu huu hufanyika kote duniani.

Hivi karibuni, zilisambaa picha za baadhi ya wanahabari wanaoendesha runinga za mitandaoni wakiwa na maafisa wa TCRA na ikaelezwa kuwa wametakiwa kusitisha kazi hiyo hadi maelekezo zaidi yatakapotolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *