Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amemteua Hassan Abbas kuwa mkurugenzi wa Idara ya habari ( MAELEZO).

Waziri Nape Nnauye: Akimtangaza Hassan Abbas kuwa mkurugenzi mpya wa Idara ya habari (MAELEZO) mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Nape Nnauye: Akimtangaza Hassan Abbas kuwa mkurugenzi mpya wa Idara ya habari (MAELEZO) mbele ya waandishi wa habari.

Hassan Abbas ambaye pia ni msemaji wa Serikali amechukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Hassah Mwambene aliyehamishiwa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari mara baada ya uteuzi huo mkurugenzi huyo amesema mikakati yake ni kuongeza mbinu za mawasiliano kati ya Serikali na wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *