Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Hussein Mwinyi amesema vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vile vya nchi jirani vimekuwa katika hali ya tahadhari kufuatilia matishio ya ugaidi wa Kimataifa.

Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018.

Pia Dkt. Mwinyi amesema kuwa kwasasa hali ya ulinzi na usalama ni shwari kutoka na majeshi kujiimarisha zaidi.

Mwinyi ameongeza kwa kusema kuwa hali ya ulinzi na usalama wa mipaka ya tanzania ipo shwari.

Pia amesema kuwa maeneo yote ya ukanda wa Afrika Mashariki, maziwa makuu na Pembezoni ya Afrika ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Somalia na Sudani Kusini pia yapo shwari.

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa uwepo wa matishio ya ugaidi wa kimataifa umelazimu vyombo vya ulizni na usalama kwa kushirikiana na nchi jirani na raia wake kuendelea kuwa na tahadhari na umakini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *