Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewashuku watanzania kwa ushirikano waliompa wakati wa msiba wa mke wake, Linah Mwakyembe kilichotokea Julai 15 kwenye Hospitali ya Aga Khan.

Mwakyembe amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Dk Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.

Pia Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela Mkoani Mbeya, amewashukuru viongozi wote wa dini akiwamo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zuberi na maaskofu.

Alimalizia kwa kusema kuwa wanafamilia tutakumbuka moyo adhimu na upendo na ushirikiano tulioupata kutoka Katibu Mkuu wa wizara hii Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *