Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesimamisha bei mpya ya ununuzi wa umeme zilizotangazwa na mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) walitangaza kuongeza asilimia 8.5 ya bei umeme kuanzia leo Januari baada ya kupokea maombi kutokana Shirika la Umeme nchini Tanesco.

Mkurugenzi mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi alitangaza ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme nchini ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19.

Taarifa iliyotolewa jana na Waziri Prof. Muhongo imeitaka EWURA kusitisha mara moja utekelezwaji wa mpango huo wa kuongeza asilimia 8.5% ya bei ya umeme, na badala yake isubili maamuzi mengine ya serikali itakapojiridhisha baada ya kupitia ripoti rasmi zote zitakazowasilishwa na EWURA, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau wote wa masuala ya nishati.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *