Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn leo anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya ziara ya kitaifa ya siku mbili ikiwa ni mwaliko wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Suzan Kolimba amesema dhumuni la ziara hiyo ni kukuza uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na kujadiliana fursa zaidi za ushirikiano katika maendeleo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Bi. Naimi Azizi amesema Ethiopia imejizatiti katika kukabiliana na changamoto ya tatizo la umeme hususani katika bara la Afrika na kwa sasa inatekeleza mradi mkubwa wa umeme ambao unaweza kusaidia baadhi ya nchi za Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *