Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn ameondoka nchini jana kurejea nchini mwake Ethiopia baada ya kumaliza ziara yake rasmi ya kiserikali.

Ziara hiyo ilikuwa maalum kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Hailemariam Dessalegn ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Akiwa nchini Hailemariam Dessalegn amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam, amehudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Dkt. Magufuli kwa heshima yake.

 Jana asubuhi ametembelea bandari ya Dar es Salaam ambapo amesema nchi yake ipo tayari kuitumia bandari hiyo sambamba na kuanzisha kituo cha huduma za usafirishaji wa mizigo kwa ndege (Cargo Hub) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kupitia shirika lake la ndege la Ethiopia Airline.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *