Serikali imesema haitasita kuwaondaoa katika nyadhifa zao wakurugenzi wote watakaoshiriki katika kutoa taarifa za uongo kuhusu miradi mbali mbali ya maendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na waziri mkuu, Kassim Majaliwa wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.

Waziri mkuu Majaliwa amesema kwamba Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakiandika taarifa za uongo kuwa mradi umekamilika wakati aujajengwa, hivyo viongozi watakaoshiriki kutoa taarifa zisizo sahihi wataondolewa.

Waziri mkuu ametoa wito kwa wakurugenzi katika halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatembelea miradi yote inayojengwa katika maeneo yao ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama thamani yake inaringana na thamani ya fendha iliyotolewa.

Waziri mkuu Majaliwa pia amesema Serikali aihitaji halmashauri kutoa ajira za mikataba kwenye kada zilizopo katika muundo wa ajira hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya mapitio ya watumishi wa mikataba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *