Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inalinda amani ya nchi kwa gharama yeyote na haitoruhusu mwanasiasa yeyote kusababisha uvunjifu wa amani hiyo.

Waziri Mkuu amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini pamoja na wazee wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.

Aliendelea kusema Serikali inataka Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato na kuwaletea tija hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu.

Pia Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wake kwa sababu kazi ya uongozi ni ngumu na inachangamoto nyingi sana.

Vile vile aliwataka viongozi wa dini hao kuharakisha uundwaji wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Rukwa.

Kwa upande mwingine waziri mkuu amesema suala la malipo kwa mawakala wa pembejeo za kilimo linafanyiwa kazi na watalipwa baada ya Serikali kukamilisha zoezi la uhakiki wa madeni hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *