Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema safari ya kuhamia Dodoma imeiva na amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wajipange kisaikolojia.

Waziri mkuu ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam ambapo amewataka watambue kuwa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kuhusu agizo hilo kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanyika ili kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo ili kufanikisha kuhamishia makao makuu ya serikali katika mkoa huo teule.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wazidishe mshikamano miongoni mwao huku wakitambua kuwa wana dhamana ya kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na uaminifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *