Waziri mkuu: Mimi nitakuwa wa kwanza kuhamia Dodoma

0
282

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema atakuwa wa kwanza kuhamia Dodoma kutokana na agizo la viongozi wote kuhamia mkoani humo.

Waziri mkuu ameyasema hayo katika maadhimisho ya kuwakumbukua mashujaa waliolipigania taifa yaliyofanyika mjini Dodoma mapema leo na kuwaambia wakazi wa Dodoma waliofika katika maadhimishi hayo kuwa mnamo mwezi wa tisa atakuwa tayari ameshahamia huko.

Pia amesema amemuita waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na katibu mkuu, amewaambia wakamilishe nyumba yake na atahamia mwezi wa tisa mwaka huu.

Waziri mkuu alisisitiza kuwa wakazi wa mkoa huo waongeze hoteli za kitalii, nyumba za kulala wageni, mahoteli makubwa ili waandae mazingira ya kupata tija kufuatia ujio wa mawaziri mbalimbali na wageni kutoka nchi mbalimbali.

Waziri mkuu aliwashukuru wote walioudhuria maadhimisho hayo na kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumpa nafasi ya kuongea na wananchi wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla.

LEAVE A REPLY