Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Jobaj, Wilaya ya Karatu mkoani Manyara unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania.

Mradi huo wenye thamani ya Sh milioni 285, ulizinduliwa juzi wakati wa ziara ya kiongozi huyo mkoani hapa na utahudumia vijiji vitatu vya Kata ya Baray ambavyo ni Mbunga Nyekundu, Jobaj na Dumbechand.

Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wananchi wautunze mradi huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania, Revocutus Kamara, alisema mradi huo unatokana na mahitaji ya maji katika vijiji hivyo vitatu na uwepo wa kisima kirefu cha maji kilichochimbwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2009.

Akizungumza kuhusu mradi wa umwagiliaji, mkurugenzi huyo alisema shirika lao limechangia kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga kilomita 1.716 za mfereji katika Kijiji cha Jobaj.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *