Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji wa madini nchini kuondoa hofu ya kukosa haki zao kwani kamati ya pili iliyoagizwa kufanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (Makinikia) bado haijakamilisha kazi yake.
Waziri mkuu amesema hayo leo wakati akijibu swali la mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka lililohoji kuhusu taswira ya Tanzania kimataifa katika ewekezaji wa madini.
Waziri mkuu Majaliwa amewaondoa hofu wawekezaji hao kwa kuwa kamati ya pili iliyoundwa kuangalia athari za kisheria, kisiasa na kimataifa kuhusu sakata la mchanga wa madini bado haijatoa ripoti yake.
Majaliwa amesema kuwa watanzania walikuwa na hofu pamoja na wabunge walikuwa na hofu kuhusu sakata la mchanga wa madini lakini Rais Magufuli alikuwa na nia njema ya kulinda rasimali ya taifa.
Waziri mkuu amewataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwani Serikali itazingatia ushauri kutoka sekta nyingine kabla ya kuchukua hatua katika sakata hilo la mchnga wa madini.