Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaonya wanaotoa matamshi ya kichochezi nchini na kusema kuwa serikali itawashughulikia bila ya kujali nyadhifa zao.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana wakati wa ibada ya mazishi ya mke wa Dkt. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe yaliyofanyika Kyela jijini Mbeya.

Majaliwa amesema kuwa “Tutashughulika na watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi, popote walipo bila ya kujali uwezo wao, vyeo vyao na mamlaka walizonazo,”.

Pia Waziri Mkuu amewaomba wananchi wote washirikiane kwa pamoja kumuombea Dkt Mwakyembe na familia yake ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *