Waziri mkuu apokea msaada wa mabati 100

0
213

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa mabati 100 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni mbili kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Lindi, Hamida Abdallah.

Msaada huo umetolewa jana katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa, wakati Waziri Mkuu alipotembelea hospitali hiyo.

Mbunge huyo amesema amekabidhi msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Aprili mwaka huu, wakati Waziri Mkuu alipofanya ziara katika hospitali hiyo..

Waziri Mkuu amemshukuru Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake na kumuomba aendelee kuisaidia hospitali hiyo pindi anapopata nafasi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema mkakati wake kwa sasa ni kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati ili kuwawezesha wananchi kupata matibabu karibu na makazi yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Andrea Chezue, alimshukuru Waziri Mkuu kwa jitihada zake za kuboresha huduma hospitalini hapo.

Amesema hivi karibuni walipokea Sh milioni 100 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa ajili ya ukarabati wa wodi mbili ambazo tayari ukarabati huo umekamilika na zitaanza kutumika kuanzia Novemba 15, mwaka huu.

LEAVE A REPLY