Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa jana ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Mzee Xavery Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwa Mheshimiwa Pinda kijijini Zuzu, Manispaa ya Dodoma  Waziri Mkuu ametoa pole kwa wanafamilia na kuwaomba waendelee kumuombea marehemu apumzike mahala pema peponi.

Mzee Xavery alifariki dunia Novemba 27, 2016 saa 9.30 alasiri katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.


Amesema msiba huo ni mzito, hivyo anawaomba wanafamilia wawe watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Wakati huo huo Waziri Mkuu alimuhakikishia Mheshimiwa Pinda kwamba Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *