Shirika la Hifadhi ya taifa ya jamii (NSSF) ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi limechanga jumla ya shilingi milioni 50 kwa ajiri ya kuchangia harambee ya ujenzi wa shule ya Sekondari iliyoungua na kuteketea kwa moto mkoani Lindi.

Harambee hiyo iliongozwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Majaliwa Kassim Majaliwa, huku meneja wa Shirika la NSSF mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz akitoa ahadi ya kutoa pesa hizo kwa Waziri Mkuu.

Watu mbali mbali waliudhuria harambee hiyo akiwemo mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete ambapo jumla ya shilingi milioni 80 zilichangwa katika harambee hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *