Waziri Mkuum wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameahidi kufanya linalowezekana ili kupunguza msongamano wa watu wanaofika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kupata matibabu.

Waziri mkuu amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kampasi ya chuo kikuu kishiriki cha afya na sayansi ya tiba Muhimbili (MUHA’S), pamoja na ujenzi wa kituo cha tiba cha kimataifa cha Muhimbili katika eneo la Mloganzila nje kidogo ya Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Majaliwa aliambatana na waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na makamu mkuu wa chuo hicho, Prof. Efatha Kaaya.

Waziri mkuu amesema Serikali itaendelea kutoa kipaumbele kukamilisha awamu yake, tutakata eneo hili liweze kuwa linatoa huduma ili kupunguza msongamano mkubwa uliopo kwenye hospitali yetu ya taifa ya Muhimbili.

Aliongeza kwa kusema kwamba wakishapunguza msongamano madaktari watafanya kazi kwa uhakika zaidi na kwa umakini mkubwa.

Pia alitoa wito kwa wizara ya elimu, kuweka mpango maalumu wa kuongeza wataalam zaidi katika sekta ya afya ili kuipunguzia serikali gharama ya kusomesha wataalamu hao nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *