Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kutafuta mbinu bora za kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ili kukuza sekta hiyo.

Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika mji wa kitalii wa Varadero ulioko kwenye mkoa wa Matanzas nchini Cuba.

Amesema mji wa Varadero tu unaingiza watalii zaidi ya milioni moja kwa mwaka na unategemea kivutio kikubwa kimoja tu cha fukwe ambayo ina urefu wa kilomita 22.

Majaliwa amesema kuwa idadi hiyo ni tofauti na Tanzania ambayo imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii huku watalii wanaovitembelea ni wachache. “Tunatakiwa kujitangaza zaidi.” alisema Majaliwa.

Waziri Mkuu alitaja baadhi ya vivutio vya utalii ambavyo ni mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, miji ya kihistoria ya Kilwa, Bagamoyo, Stone Town pamoja na Mikindani.

Pia Waziri Mkuu aliwahamasisha Watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio vyeo vya utalii na kujifunza mambo mbalimbali na si kuwaachia wageni pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *