Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuboresha mikakati yake kwa ajili ya kudhibiti uchimbaji na biashara ya madini nchini ili kuleta tija kwa maendeleo.

Miongoni mwa mikakati hiyo, ni kuvutia wawekezaji, kuandaa wataalamu na kuboresha mifumo.

Majaliwa aliyasema hayo jana wakati wa Mkutano wa 37 wa Mawaziri wa Nishati na Madini wa nchi wananchama wa Kituo cha Madini cha African Minerals and Geoscience Centre (AMGC), licha ya mambo mengine ulijadili mchango wa sekta ya madini kwenye uchumi wa Afrika.

Waziri mkuu alisema licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa wa madini, sekta hiyo haina tija kwenye maendeleo ya uchumi kwa wananchi wake hasa waishio karibu na migodi.

Alisema hivi sasa hali hairidhishi kwa kuwa maeneo mengi ya machimbo yameharibiwa, huku wakazi wake wakiachwa maskini.

Pia, alihimiza kutumia kituo hicho kwa ajili ya kufanya utathmini na uongezaji thamani wa madini nchini, badala ya kuyasafirisha yakiwa ghafi.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema aliagiza kampuni za madini na wachimbaji wadogo mwakani zitaanza kupeleka madini kwa ajili ya kufanya tathmini ya viwango, badala ya kuyasafirisha nje ya nchi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *