Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasimu Majaliwa ameahirisha Bunge leo hadi Novemba 7 mwaka huu.

Wakati wa kuahirisha Bunge hilo waziri mkuu amefafanua kuhusu hali ya wakulima na changamoto wanazokumbana huku akielezea mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano inavyopambana na changamoto kwa lengo la kukuza kipato cha mkulima.

Majaliwa amelieleza Bunge kuwa serikali imechukua jitihada za dhati za kuwataftia masoko wakulima pamoja na kupunguza tozo la kodi mbalimbali kwenye mazao.

Waziri Mkuu amewasihi wazazi na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza sekta ya Elimu nchini.

Majaliwa pia ameeleza kuwa serikali inafanya jitihada kubwa kuwezesha sekta ya vijana na hususani kuwasadia katika kupata ajira.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Majaliwa aliwashukuru wabunge wote wa bunge hilo tukufu na kutoa hoja ya kuahilisha Mkutano wa Nane wa Bunge hadi Novemba 7, 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *