Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mbeya kuwakamata, kuwahoji na kisha kuwafikisha mahakamani viongozi wa wa jiji hilo kwa ubadhirifu na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 63.

Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa waliowahi kuwa wakurugenzi watatu na Kaimu Mkurugenzi mmoja wa Jiji la Mbeya.

Wengine ni Meya Mstaafu wa jiji hilo, wahasibu wawili na wajumbe wote wa bodi walioshiriki kuidhinisha fedha za Mradi wa Soko la Mwanjelwa kwa kuisababishia hasara kubwa halmashauri ya jiji hilo.

Agizo hilo limekuja kufuatia kuongezeka gharama za ujenzi wa soko hilo kutoka shilingi bilioni 13 hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni 19 na hivyo halmashauri kutakiwa kulipa deni hilo na riba inayofikia zaidi ya shilingi bilioni 63.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *