Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba kuifanyia marekebisho makubwa Bodi ya Korosho na menejimenti yake baada ya kushindwa kusimamia zao hilo ipasavyo.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea mkoani Lindi ambapo amesema Serikali itafanya mapitio ya bodi zote za mazao ya biashara.

Amesema serikali imeanza na zao la korosho kisha zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai.

Katika tathmini na mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa kutekeleza majukumu yake itavunjwa.

Amesema anaishangaa bodi hiyo kuacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia minada ya korosho na kuzuia baadhi ya wafanyabiashara wasiweze kununua zao hilo hali inayoashiria kuwepo kwa watu waliopangwa kununua bila ya kufuata utaratibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *