Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mjini.

Profesa Mbarawa amesema hayo katika uzinduzi wa treni itakayofanya safari kuanzia stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu huku akisema kuanza kwa usafiri huo umepunguza dala dala 45.

Waziri Mbarawa amesema kwamba serikali inahakikisha inapunguza msongamano wa magari na ikiwezekana kumaliza kabisa msongamano huo katika jiji la Dar es Salaam huku akisema pia serikali inataka kuanzisha usafiri wa majini ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Vile Vile waziri amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa  mazoea kwani ikitokea wafanyakazi wazembe watashughulikiwa ipasavyo.

Pia amewataka wanacnhi waliojenga pembeni mwa reli wabolewe haraka kwani sheria airuhusu kujenga maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *