Serikali imesema kuwa sababu iliyofanya watanzania kufukuzwa nchini Msumbiji ni kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo.

Hayo yamesemwa na waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipokuwa anaongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Balozi Mahiga alisema Tanzania imekuwa na ushirikiano na Msumbiji kwa muda mrefu hivyo utaratibu walioufuta wa kuwaondoa wahamiaji hao ni wa kiuungwana.

Pia amesema kuwa mawaziri wa nchi 14 walianza kuwasili nchini kwa ajili ya kikao cha mawaziri ambacho Tanzania ni mwenyekiti wao, na siyo kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya Msumbiji, ila yenyewe ni nchi jirani na watazungumzia masuala ya ulinzi na usalma na ushirikiano wa nchi hizi za SADC.

Amesema watu hao ambao waliingia Msumbiji bila kufuata taratibu, wakiwa huko pia wamevunja sheria za nchi hiyo kwa kujihusisha shughuli bila vibali na kinyume cha taratibu za ajira za nchi hiyo sanjali na kujiingiza katika vitendo vya uhalifu mbaya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *