Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amefuta vibali vyote vya uwindaji kwa kampuni kuanzia jana na kutoa siku 60 kwa watendaji ili waratibu mchakato upya utakaowezesha vitalu kugawiwa kwa mnada.

Dk Kigwangalla pia amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, ndani ya muda mfupi kuwaandikia Hazina ili kuzichukua hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa ambazo zimeshindwa kutimiza masharti.

Ametoa maagizo hayo jana alipohitimisha mazungumzo na wadau wa sekta ya utalii na maliasili aliokutana nao mjini  Dodoma.

Kuhusu vitalu vyenye migogoro vikiwemo vya Loliondo na Natroni, ameagiza visigawiwe hadi migogoro itakapokwisha.

“Kwenye hili la hoteli, nataka katibu uwasiliane na mamlaka husika, ikiwemo Msajili wa Hazina ili ndani ya siku 60 uje na majibu tutangaze kwa wawekezaji watakaokwenda na masharti,” amesema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *