Waziri Kairuki azindua safari ya Dodoma kwa watumishi wa wizara yake

0
251

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi ya Umma na Utawala bora, Angella Kairuki amezindua safari ya kwanza ya wizara hiyo kuelekea makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.

Uzinduzi huo umefanywa leo jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za wizara hilo kwa lengo la kutimiza matakwa ya Rais Magufuli ya Serikali yote kuhamia mkoani Dodoma ifikikapo Februari 28 mwaka huu.

Wakati wa uzinduzi wa safari hiyo waziri Kairuki amesema kuwa kundi la kwanza lina jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.

Pia amesema kwa mahitaji na ofisi hiyo ikiwa pamoja na kukutana na waziri kuhusu masuala sera na sheria za utumishi wa umma na utawala wa utumishi wa umma yatatekelezwa katika ofisi za Dodoma zilizopo katika jengo la College of Hummanities and Social Sciences ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma mkoani humo.

LEAVE A REPLY