Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limemtaka rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kufuatia kauli aliyoitoa kwenye Sala ya Eid el Fitr, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Jumatatu iliyopita Juni 26.

Katika sala ya Eid, mzee Mwinyi alisema anamkubali sana rais Magufuli kwa jinsi anavyoinyoosha nchi, na kusema kama isingekuwa kubanwa na katiba, alitakiwa aachwe atawale milele.

Kwa kauli moja, wazee hao wamewataka wazee wenzao wa CCM, kukaa na mzee Mwinyi na kumuonya kuhusu kauli zake hizo, huku wakiwataka pia wazee wa CCM, kukaa na Rais Magufuli na kumuonya Mwinyi kwa sababu matamshi yake ni kinyume kabisa na katiba.

Kwa upande wake, Profesa Baregu, alisema mzee Mwinyi amewahi kusema nchi inavyoongozwa ni kama gari lisilo na usukani, akahoji iweje abadilishe mawazo yake na kuanza kuzungumza lugha tofauti, akijifanya anamkubali Rais Magufuli?

Naye Arcado Ntagazwa, alisema wananchi wote wanampongeza Rais Magufuli kwa sasa lakini hawajui matokeo ya maamuzi anayoyafanya leo kesho yatakuwaje na je, kesho atatoa maamuzi gani?.

Source: Global Publishers

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *