Hukumu ya kesi inayomkabili muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ya kuua bila kukusudia, inatarajiwa kutolewa Novemba 13 mwaka huu.

Kesi hiyo ambayo imesikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema imemkuta Elizabeth Michael na hatia ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake, baada ya kusikiliza maoni ya Baraza la Wazee hii Leo.

Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.

Kabla ya  wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo ya Baraza la Wazee.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa dhidi ya muigizaji huyo wa Bongo Movie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *