Watu 11 wamenusurika kifo baada ya kufukiwa na kifusi mgodini wakati wakichimba dhahabu kwenyemgodi wa Buhemba wilayani Butiama mkoaoni Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi amesema kazi ya uokoaji inaendelea kwa ajili ya kuwatafuta watu wengine ambao ndugu zao hawajawaona na wanahisi walikuwamo ndani ya shimo hilo.

Amesema mmomonyoko wa udongo ndiyo uliosababisha kuporomoka kwa mashimo hayo ya muda mrefu licha ya kuwapo jua kali.

Pia amkuu Wilaya huyo amesema kuwa mashimo hayo yaliyoachwa na mkoloni yako chini ya mwekezaji StanCom ambaye ndiye aliyekuwa akichimba dhahabu katika eneo hilo.

Kwasasa wachimbaji waliookolewa wamepelekwa Hospitali ya wilaya kwa ajili ya matibabu kutokana na ajali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *