Katibu Mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa wizara hiyo imeanza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuhamia mjini Dodoma kabla ya Februari mwakani.

Profesa Mchome amesema kuwa awamu ya kwanza ya watumishi wa wizara hiyo inategemea kuondoka jijini Dar es Salaam Januari kwenda mkoani Dodoma.

Pia Katibu huyo amewataka watumishi wote wa wizara hiyo kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma kabla Januari.

Awali, tangazo la wizara hiyo lilisambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu orodha ya watumishi wake wanaohamia Dodoma kuwa ipo tayari na wataondoka Januari.

Vile vile Profesa Mchome amesema mambo mengine ni ya ndani na asingependa kuyazungumza wazi lakini alisisitiza kuwa, kikubwa kuhamia Dodoma ni lazima na itafanyika kwa awamu hadi kukamilika mwaka 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *