Jeshi la polisi nchini limetoa orodha ya majina 12 ya wanaotuhumiwa kuratibu na kuendesha harakati na mauaji ya viongozi wa serikali za vijiji katika wilayani Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amesema kupatikana kwa watuhumiwa hao pamoja na picha ni kutokana na oparesheni inayoendelea na vyombo vya ulinzi katika Wilaya hizo.

Lyanga amesema kuwa wameweza kuwabaini watuhumiwa wa mauaji hayo, Watuhumiwa hao wameweza kubainika kwa majina na picha kwa baadhi yao ni matokeo ya oparesheni inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraji Ismail Nangalava, Anaf Rashid kapera, Said Ngunde, Omary Abdalla Mandimbwa, Shaban kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Njame, Rashid Salum Mtulula, Shekhe Hassan Nasri Mzuzuzi, Hassan Uponda,” alisema Kamanda Lyanga.

Pia amesema kuwa jeshi la polisi limebaini haya kushirikiana na wasiri wao huku wakiendelea na uchunguzi zaidi.

Jeshi hilo limetoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kufichua kwa siri watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama katika mkoa huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *