Watu 12 wanahofiwa kufariki dunia baada ya mashua iliyokuwa safarini kutoka mji wa wa Tanga ikielekea visiwa vya Pemba kuzama Jumatatu usiku.

Kamanda polisi eneo la kaskazini mashariki, Benedict Wakulyamba amesema kuwa mashua hiyo ilikuwa imewabeba watu 50.

Mkuu huyo wa Polisi amesema kuwa watu tisa wameokolewa na miili 12 kupatikana baada ya kutokea ajali hiyo.

Kilichosababisha kutokea ajali hiyo hakijathibitishwa lakini kamanda wa polisi anasema upepo mkalia huenda ulisababisha mashua hiyo kupoteza mwelekeo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *