Watu zaidi ya 140 wamekufa baada ya tetemeko la ardhi kubwa kuikumba nchi ya Mexico siku ya jana.

Tetemeko hilo linalodaiwa kuwa na ukubwa wa 7.1 limeanguja nyumba zaidi ya 30 katika mji wa Mexico City na watoto 30 hawajulikani walipo.

Baada ya kutokea janga hilo, rais wa nchi hiyo Enrique Peña Nieto amesema kuwa wanakabiliwa na dharura ya taifa lao.

Pia Rais wa Marekani, Donald Trump ametuma salamu zake za pole kwa nchi hiyo kupitia mtandao wa Twitter kwa kuandika, “God bless the people of Mexico City. We are with you and will be there for you.”

Wakati huo huo tetemeko hilo limesababisha madhara katika majimbo ya mengine ya karibu kama Morelos na Puebla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *