Watu wenye vipara wameuawa nchini Msumbiji kutokana na imani za kishirikina zinazofanywa na wauaji hao.

Wauaji hao wanaamini kuwa watu wenye vipara wanadhahabu kwenye vipara vyao ndiyo mana wanawaua ili kupata utajiri kwa njia za kishirikina.

Hadi sasa Polisi katika jimbo la Zambezia nchini Msumbiji wamewakamata watu wa nne kwa kuhusika na mauaji ya watu wenye vipara.

 Pia Polisi hao wanaendelea na uchunguzi huku wakifuatilia zaidi kujua nani anachochea mauaji hayo kwa watu hao wenye vipara nchini humo.

Waganga wa kienyeji wamekuwa wakidaiwa kusambaza habari zisizo na ukweli kwamba vichwa vya watu wenye vipara vimekuwa na dhahabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *