Watu wawili wamefariki na wengine 16 wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi baada ya kutokea shambulio kwenye klabu ya usiku katika mji wa Florida nchini Marekani.

Shambulio hilo limetokea katika mji wa Fort Myers, Florida ambapo klabu hiyo ilikuwa imeandaa tamasha kwa ajili ya vijana.

Majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa kutumia magari ya kuwabeba wagonjwa kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.

Polisi nchini humo bado wanajaribu kubaini chanzo cha ufyatuaji risasi huo katika klabu hiyo ya usiku huku wakimkamata mtu mmoja kwa ajili ya mahojiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *