Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Mwanza kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea.

Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo ambapo kwa sasa usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa.

Sianga amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na moto huo huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na mapambano kila siku na kwamba hata leo, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za kulevya amekamatwa.

 Kamishna Sianga amesema hatatumia njia hiyo kwa kuwa kutaja majina ya watu hadharani kunaweza kuiingiza serikali katika matatizo maana kuna watu wengine wanaweza kutoa majina ya watu kwa sababu ya chuki binafsi.

Amesema njia anayoitumia ni kuwakamata na kuwahoji kimyakimnya na wakishajiridhisha hatua nyingine za kisheria zinafuata.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *