Watu zaidi ya 20 wameuawa na huku wengine 24 wamejeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha moja huko Las Vegas.

Mtu mwenye silaha alifyatua risasi katika tamasha moja la muziki wenye hoteli ya Mandalay Bay mjini humo.

Mamia ya watu walikimbia eneo hil na milio ya risasi ilisika kwa muda kwenye video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Ufyatuaji huo ulitokea wakati wa tamasha hilo na walioshuhudia walisema kuwa mamia ya risasi zilifyatuliwa.

Usafiri wa ndege umesitishwa kutoka uwanja wa ndege wa McCarran mjini Las Vegas kutokana na tukio hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *