Watu wanne wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyamalinde kijiji cha Sobola mkoani Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu.

Kamanda huyo amesema kuwa tukio hilo limetokea  jana majira ya saa mbili asubuhi katika machimbo hayo yanayomilikiwa na wananchi licha ya kuwa tayari yalishapigwa marufuku kuendelea kwa kazi hiyo.

Mponjoli amesema tukio hilo limetokea baada ya watu 7 kuingia ndani ya mgodi huo, lakini muda mfupi baadaye kifusi kikawaangukia na kusababisha vifo vya watu wanne kati yao huku watatu wakitoka salama licha ya kuwa na majeraha.

Amewataja watu waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na Robert Kazegemwa, Jeremia Emmanuel, Makenya Mwita na Julius Timotheo.

Waliojeruhiwa ni pamoja na Mashaka Samuel, Justine Safari na Maneno Lusika ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Katoro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *