Watu watatu wakazi Ilemela Mkoani Mwanza wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na dawaza kulevya aina ya ‘heroine’ kiasi cha pinchi 10 pamoja na bangi yenye misokoto inayokadiriwa kufika 52.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP, Zarau Mpangule amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ally Salehe (47), mkazi wa Nyasaka, Wiliam Magoma (31) mkazi wa Nyasaka ambao walikamatwa wakiwa na bangi huku Paschal Lusozi (47) mkazi wa Nyasaka yeye alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroine.

Taarifa zinaeleza kuwa askari waliokuwa kwenye doria na misako waliweza kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba katika mtaa wa sabasaba wapo baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, ndipo askari walipoanza kufanya upelelezi na misako katika maeneo hayo na kuwatia nguvuni watuhumiwa hao.

Pamoja na hayo Kamanda Mpaungule amesema Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na watuhumiwa wote watatu, pindi uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani, na kuongeza kwamba upelelezi na msako wa kuwatafuta watu wengine wanajihusisha na biashara haramu za dawa za kulevya bado unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *