Watu watano wamefariki na wengine sita kujeruhiwa baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe katika mgodi wa zamani wa Resolute uliopo Nzega, Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla amesema kuwa tokea hilo limetokea juzi saa saba mchana baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo lililopigwa marufuku na Serikali.

Ngupulla amesema eneo hilo limeshapigwa marufuku kuchimbwa kutokana na hatari iliyopo lakini baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiingia kwa kificho kuchimba hali iliyosababisha kuleta maafa.

Amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Mpenda ambaye ni mkazi wa Shinyanga, Mohamed Mohamed, mkazi wa Singida, Manona Nyombi, mkazi wa Bariadi, Modesta Leonard, mkazi wa Nzega na mwingine bado hajatambulika.

Almewataja majeruhi kuwa ni Kangwa Mayenga (22) ambaye ni mkazi wa Bariadi, Agness Antony (40), mkazi wa Chato, Deus Alphonce (45), mkazi wa Igunga na Mathias Mapunda, mkazi wa Chato.

Amesema majeruhi wote kwa pamoja wanaendelea kupata matibabu na wawili ambao majina yao hayakupatikana kutokana na kuwa mahututi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *