Dereva wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumkata kwa mapanga usiku wa kuamkia leo majira ya saa 2 usiku huku ikielezwa kuwa hali yake siyo nzuri.  

Taarifa hizo za kusikitisha zimethibitioshwa na Bosi wa Dereva huyo ambaye ni Mbunge John Heche kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri kuwa dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku ambapo dereva wa mbunge huyo alivamiwa na kushambuliwa vibaya kwa mapanga.

Katika uvamizi huo ameshambuliwa kwa kukatwa katwa na mapanga kichwani na hali yake si nzuri, anaendelea na matibabu kwenye Hospitali ya Bomani Tarime.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *